Shirika La Afya Duniani Kuchunguza Dawa Za Mitishamba Kwaajili Ya Tiba Ya Corona

Dawa za asili
Shirika la afya ulimwenguni WHO na kituo cha udhibiti wa magonjwa barani Afrika CDC yameanzisha juhudi kuangalia uwezekano wa madawa ya mitishamba katika kupambana na janga la virusi vya corona. 

Jopo hilo jipya la ushauri litaunga mkono nchi katika majaribio ya kitabibu, utafiti mwingine na utengenezaji wa dawa nyingine za kienyeji wakati hivi sasa janga likisambaa kwa kasi katika baadhi ya sehemu za bara la Afrika. 

Kesi zilizothibitishwa katika bara hilo zimekaribia kufika 750,000, zaidi ya nusu zikiorodheshwa nchini Afrika kusini.

Taarifa ya WHO imesema dawa za asili, zina faida nyingi na bara hilo lina historia ndefu ya matumizi yake. 

Mkuu wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti amesema utafiti inapaswa kuwekwa katika misingi ya kisayansi.

Mataifa kadhaa yalionesha shauku baada ya rais wa Madagascar kutangaza dawa ya mitishamba kama sehemu ya taifa hilo la kisiwani kupambana na janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon