Shirika La Afya Duniani Limeeleza Wasiwasi Wake Kuongezeka Maambukizi Ya Corona Ulaya

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza wasiwasi wake juu ya kuzuka wimbi lingine la maambukizi ya virusi vya corona barani Ulaya. 

Kulingana na shirika la habari ya AFP, humusi moja ya maambukizi yote milioni 15 duniani, yametokea barani Ulaya. Ni bara liloathirika zaidi likiwa na vifo zaidi ya 207,000 vilivyotokana na virusi hivyo, kati ya 633,711 vilivyotokea ulimwenguni kote. 

Shirika la WHO limesema kumeongezeka maambukizi barani Ulaya katika wiki mbili zilizopita, likisisitiza haja ya kuchukua hatua zaidi, iwapo itahitajika. 

Msemaji wa WHO barani Ulaya amesema ongezeko hilo la maambukizi ya virusi vya corona, linawapa wasiwasi hasa kwa vile limetokea baada ya hatua za kujikinga kulegezwa katika baadhi ya mataifa barani humo.


EmoticonEmoticon