Tory Lanez Akamatwa Na Polisi Na Kufunguliwa Mashtaka Haya

Tory Lanez
Tory Lanez anashikiliwa na polisi mara baada ya gari lake kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

Sekeseke lilianza baada ya polisi kufika kwenye nyumba moja mjini Hollywood Hills ambapo kulikuwa kunafanyika 'house party' kelele zilikuwa kibao ndipo majirani walipiga simu polisi, baada ya kuwasili walikuta vurugu na watu wakizozana kwenye gari punde ulisikika mlio wa risasi na gari hilo kuondoka.

Polisi walipata taarifa za gari hilo na kuanza kulifuatilia, walifanikiwa kulikamata na ndani walimkuta Tory Lanez na mwanamke ambaye ni Megan Thee Stallion.

Megan alikuwa ameumizwa kwenye mguu wake ambapo inadaiwa kuwa alikatwa na vioo vilivyovunjika toka kwenye paa la gari baada ya risasi kupigwa juu. Baada ya upekuzi polisi walikuta silaha kwenye gari hilo.

Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba mwimbaji huyo na rapa toka nchini Canada [Tory Lanez] alifikishwa kituo cha polisi na kufunguliwa shtaka la jinai kwa kuficha silaha ndani ya gari.


EmoticonEmoticon