Trump Amtetea Daktari Mwenye Njama Anazodai Zina Mvuto Kuhusiana Na Corona

Stella Immanuel, Trump
Stella Immanuel ni dakatari ambaye amekuwa chanzo cha mkanganyiko kuhusu madai ambayo hayajathibitishwa kuhusu dawa ya malaria kuwa na uwezo Covid- 19.

Facebook na Twitter zimeondoa video ambayo daktari huyo alikuwa akionekana, makampuni hayo yakisema kuwa video hiyo imekiuka sera ya taarifa za kupotosha- lakini kabla ya hayo ilikuwa imechapishwa tena na Donald Trump na mmoja wa watoto wake wa kiume.
Rais wa Marekani alijitetea, pia akimsifu daktari huyo mzaliwa wa Cameroon na aishiye mjini Houston jimbo la Texas.
Trump alisema: ''Alisema amepata mafanikio makubwa baada ya kuwatibu mamia ya wagonjwa wa Covid-19, nilifikiri sauti yake ni sauti muhimu lakini sijui chochote kumhusu,'' alisema siku ya Jumanne.
Credit: Bbc


EmoticonEmoticon