Trump Afuta Kongamano La Chama Cha Republican Kwa Kuhofia Maambukizi

Donald Trump
"Huu sio wakati mwafaka wa kufanya hivyo," alisema, na kuongeza kwamba bado atatoa hotuba aliopanga kwenye mkutano huo kwa njia tofauti.

Baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican wataendelea kukutana Charlotte, North Carolina, eneo ambalo mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika awali.
Bwana Trump alikuwa amehamisha sehemu ya mkutano huo Florida kwasababu ya kanuniza kutokaribiana zilizoanzishwa North Carolina.
Katika tukio hilo la nusu siku, Agosti 24, rais atachaguliwa rasmi na chama chake kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama katika uchaguzi wa urais unaofanyika Novemba.
Katika mkutano kuhusu taarifa za ugonjwa wa virusi vya corona, akiwa Ikulu ya Marekani Bwana Trump, Alhamisi amesema kwamba usalama ndio angalizo lake kuu huku akitoa wito wa kufutiliwa mbali kwa matamasha manne ya usiku.

"Ni dunia tofauti, na hali hii itaendelea kwa muda kidogo," rais alisema akiongeza kwamba "alihisi kufanya hivyo itakuwa makosa" kuhatarisha maisha ya maelfu ya watu.
"Hatukutaka kuhatarisha maisha hata kidogo," aliwaambia wanahabari. "Ni lazima tuwe waangalifu. Lazima tuwe makini na ni lazima tuwe mfano wa kuigwa na wengine."
Ofisi ya Jacksonville sheriff shirika la kaunti linalosimamia utekelezaji wa sheria lilionya wiki hii kwamba mji huo hauko tayari kwa mkutano mkubwa wa kisiasa uliopangwa kufanyika mwzi ujao.

Florida - jimbo muhimu katika matumaini ya kuchaguliwa tena kwa rais kwenye uchaguzi wa urais - uko nyuma tu ya California na New York kwa idadi jumla ya maambukizi ambayo imerekodiwa.
Bwana Trump alibadilisha eneo la kufanyia mkutano hadi Florida baada ya gavana wa chama cha Democratic wa North Carolina kusisitiza mwezi Mei umuhimu wa kupunguza mikusanyiko katika mkutano ulipangwa kufanyika wa chama cha Republican akitaja suala la kutokaribiana.
Kura za maoni zinaonesha kwamba Bwana Trump anakibarua kigumu cha kufanya wakati anawania kuingia madarakani kwa muhula wa pili huku akiendelea kukosolewa na jinsi anavyoshughulikia janga la virusi vya corona.


EmoticonEmoticon