Uganda Yatangaza Siku Tatu Za Maombolezo Ya Raisi Mstaafu Benjamini Mkapa

Yoweri Museven
Kufuatia kifo cha rais wa awamu ya tatu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hayati Benjamin William Mkapa mnamo tarehe 24/7/2020 jijini Dar Es Salaam, viongozi wengi wa matatifa mablimbali wametuma salamu za rambirambi.

Rais wa Uganda Yoweri Museven ametuma salamu zake za rambirambi wa kusema kuwa
“Kwa masikitiko makubwa nimehuzunishwa na kifo cha kaka yetu Benjamin Mkapa, Nilianza kufanya nae kazi na H.E Mkapa mnamo mwaka 1967 wakati tulikuwa wanafunzi wa chuo kikuu na alikuwa mhariri mkuu wa gazeti la Nationalist.”
Yoweri Museven Tweets
Natuma salamu zangu binafsi za rambirambi na kwa niaba ya Watu wa Uganda kwa Anna Mkapa, Watoto na Watanzani wote, Bendera Uganda zitapepea nusu mlingoti kwa siku 3 kuanzia Jumamosi (leo) July 25 saa kumi na mbili”.


EmoticonEmoticon