Wakurugenzi Wakuu Wa Makampuni Makubwa Apple, Facebook, Amazon Na Google Kukutanishwa Pamoja

Apple, Amazone, Google, Facebook
Wakurugenzi Wakuu wa kampuni kubwa za Tech - Mark Zuckerberg (Facebook), Jeff Bezos (Amazon), Tim Cook (Apple) na Sundar Pichai (Alphabet ambayo ndio inamiliki Google) watakwepo pamoja mbele ya kamati (𝙝𝙪𝙚𝙣𝙙𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙖𝙠𝙪𝙩𝙖𝙣𝙖 𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙟𝙪𝙢𝙗𝙚 𝙖𝙢𝙗𝙖𝙤 𝙨𝙞𝙤 𝙬𝙖𝙩𝙪 𝙬𝙖𝙯𝙪𝙧𝙞). 

Wakurugenzi hawa wamepangwa kuketi mbele ya Kamati na baraza kuu la majaji, juu ya Utengenezaji wa Sheria na kudhibiti ukuaji wa makampuni makubwa ya tech kutumika vibaya.

Mada kuu ni kuhusiana na usalama wa taarifa za watumiaji kwa sababu kampuni hizi zinamiliki taarifa nyingi za watumiaji na tayari kuna changamoto nyingi kuonyesha kuwa taarifa za watumiaji zinatumia vibaya. 

Pia kampuni ndogo za tech zimelalamika kuibiwa idea na mawazo yao na kampuni kubwa na issue nyingine critical ni kuhusu namna ya kampuni hizi kubwa za Tech kudhibitiwa kwa sababu zinakua kwa kasi na inahatarisha ushindani na utawala wa sheria.


EmoticonEmoticon