Washukiwa Wa Kifo Cha Pop Smoke Huwenda Wakahukumiwa Kifo

Wiki iliyopita washukiwa wanne wa mauaji ya Pope Smoke walitiwa nguvuni na polisi. 

Sasa kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka kwenye ofisi ya mwanasheria wa wilaya, imeelezwa kwamba washukiwa hao wote wameshtakiwa kwa kosa la mauaji.

Miongoni mwa washukiwa hao, wawili ni watu wazima ambao wamefahamika kwa majina ya Keandre Rogers (18) na Corey Walker (19) na wengine wawili ni vijana wadogo chini ya umri wa miaka 18. 

Hivyo Rogers na Walker huwenda wakahukumiwa kifo au kifungo cha maisha gerezani.

Baada ya kukamatwa, washukiwa hao waliiambia idara ya polisi kwamba hawakuwa wanamfahamu rapa Pope Smoke, na walipata anuani ya kufika nyumbani kwake kwa kuiona mtandaoni mara baada ya Pope kuianika Facebook.


EmoticonEmoticon