WHO : Covid 19 Ni Suala La Afya La Dharura Kubwa Kabisa Kuwahi Kutangazwa Duniani

Covid 19 ni suala la afya la dharura kubwa kabisa kuwahi kutangazwa duniani na Shirikala afya duniani, WHO, kiongozi wake amesema.

Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa atakuwa na mkutano na kamati ya dharura ya WHO juma hili kwa ajili ya kufanya tathimini.
Kumekuwa na dharura nyingine zilizowahi kutangazwa kama vile milipuko miwili ya Ebola, Zika, polio na mafua ya nguruwe.
Zaidi ya watu milioni 16 wameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona tangu mwezi Januari na vifo zaidi ya 650,000.
''Nilipotangaza kuwa hili ni suala la dharura januari 30 kulikuwa na maambukizi chini ya 100 nje ya China, na hakukuwa na ripoti za vifo''. Alisema Dkt Tedros.
Covid 19 imebadili dunia yetu. Imewaleta watu, jumuia na mataifa pamoja, na kuwatawanya.''
Idadi ya maambukizi, aliongeza, imepanda mara mbili zaidi majuma sita yaliyipita.
Ingawa ulimwengu umefanya jitihada kubwa kupambana na virusi, bado kuna ''safari ndefu ngumu mbele yetu,'' alisema.
Katika mkutano wa Jumatatu uliofanyika mjini Geneva, WHO pia imesema kuwa kuzuia safari hakuwezi kuwa suluhu ya muda mrefu, na nchi zinapaswa kuchukua hatua zaidi kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona kwa kufuata njia zilizothibitishwa kufanya kazi kama kutocangamana na kuvaa barakoa.

''Haitawezekana kwa nchi kufunga mipaka yao. Uchumi lazima ufunguliwe, watu wanapaswa kufanya kazi, biashara zifunguliwe,'' Mkurugenzi wa program wa WHO, Mike Ryan alisema.
Maafisa wa WHO wanatambua hatahivyo, masharti ya kutotoka nje kwa nchi kadhaa zinazokabiliwa na milipuko mipya.
WHO yasema haijawahi kupata 'dharura mbaya ya kiafya' sawa na corona.


EmoticonEmoticon