Alichokisema Mwanamke Mweusi Ambaye Ni Mgombea Mwenza Marekani Baada Ya Kutokea Kwenye Kampeni Kwa Mara Ya Kwanza

Mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha Democrats nchini Marekani Kamala Harris ametokea kwa mara ya kwanza kwenye kampeni za urais za Joe Biden hapo jana, kwa kumkosoa rais Donald Trump kwa kushindwa kulikabili vilivyo janga la virusi vya corona. 

Siku moja baada ya Biden kumteua, Harris na Biden wameshikishana historia ya mahusiano baina ya familia zao na ajenda kuelekea ikulu ya White House.

Harris, seneta wa California mara moja alianza kumshambulia Trump akisema amewaingiza hatarini Wamarekani kwa kushindwa kulichukulia kwa umakini janga hilo na kuitumbukiza Marekani kwenye mzozo wa kiuchumi, katika wakati ambapo inapambana na kukosekana kwa usawa wa rangi na kijamii.

Alisema, "Huu ni wakati wa matokeo halisi kwa Marekani. Kila kitu kilicho muhimu kwetu, uchumi wetu, afya, watoto wetu na aina ya taifa tunalosihi, kila kitu kipo kwenye mstari. Tuko katika mzozo mbaya kabisa wa kiafya wa karne. Rais ameshindwa kushughulikia janga hili na kututumbukiza kwenye mzozo mbaya kabisa wa uchumi kuwahi kutokea tangu mdororo mkubwa kabisa wa uchumi."


EmoticonEmoticon