Bangi sio nzuri kwa Moyo wa binadamu, hii ni kwa mujibu wa tafiti kutoka The American Heart Association.
Taarifa hiyo mpya
ya kisayansi kutoka chama hicho cha masuala Moyo nchini Marekani imetolewa Jumatano
ya wiki iliyopita ambapo Daktari Rose Marie Robertson amesema
"The American
Heart Association inapendekeza kwamba watu wasivute kitu chochote ikiwemo
bidhaa za bangi kwa sababu ya uwezo mkubwa wa madhara kwenye Moyo, mapafu na
mishipa ya damu." alisema Dr. Rose Marie Robertson ambaye ni afisa
msaidizi wa masuala ya Sayansi na tiba kutoka The American Heart Association.
EmoticonEmoticon