China Yawawekea Vikwazo Wanasiasa 11 Wa Marekani

China imetangaza vikwazo ambavyo havijatajwa wazi dhidi ya wanasiasa 11 wa Marekani na wakuu wa mashirika yanayochochea demokrasia. 

Miongoni mwa wanasiasa hao wamo maseneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao tayari walishawekewa vikwazo na China. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Zhao Lijian, amesema wanasiasa hao 11 wamefanya vibaya katika masuala yanayohusiana na Hong Kong, ambako China imekuwa ikikandamiza upinzani tangu ilipoanzisha sheria ya usalama wa taifa. 

Idadi hiyo ya wanasiasa wa Marekani inalingana na orodha ya maafisa wa Hong Kong na China waliowekewa vikwazo na Marekani wiki iliyopita, kwa madai ya kukandamiza uhuru kisiwani Hong Kong akiwemo kiongozi wa kisiwa hicho. 

Ikulu ya Marekani White House imesema Rais Donald Trump ataendelea na msimamo wake dhidi ya China, licha ya nchi hiyo kulipa kisasi.


EmoticonEmoticon