Corona Yashusha Hali Ya Uchumi Duniani

Kama ilivyotokea Ujerumani, Ufaransa, na Uhispania, Italia nayo sasa imetangaza kushuka kwa uchumi wake kwa sababu ya janga la virusi vya corona, kwa mujibu wa ofisi zao za takwimu.

Ufaransa ilirekodi kuporomoka kwa asilimia 13.8 ya uchumi wake katika robo ya pili ya mwaka, huko Uhispania, thamani jumla ya bidhaa zinazozalishwa imepungua kwa asilimia 18.5, hiki ni kiwango kikubwa mno katika historia ya Nchi hiyo.

Italia pia inapambana na uchumi uliosinyaa kwa asilimia 12.4., Ujerumani imetangaza kushuka kwa karibu asilimia 10 ya uchumi wake, na Marekani imeshuhudia kuanguka kwa uchumi wake kwa theluthi moja.


EmoticonEmoticon