Facebook Yampa Onyo Rais Trump Kuhusu Ujumbe Wake, Twitter Yamfungia Akaunti

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeifungia kabisa akaunti ya kampeni za Rais wa Marekani Donald Trump.

Kampuni hiyo inayotoa huduma ya ujumbe mfupi imesema hatua hiyo imetokana na uchapishaji wa habari za uongo kwenye akaunti hiyo kuhusu janga la Corona.

Akaunti hiyo itafunguliwa tena tu kama ujumbe huo utafutwa. Ujumbe huo unadai kuwa watoto kwa kiasi kikubwa wana kinga ya virusi vya Corona.

Washauri wa Marekani wa afya wamesema wazi kuwa watoto hawana kinga kwa virusi vya corona. Ilikua ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii kuchukua hatua ya kuondoa ujumbe uliotumwa na rais kwa misingi ya sera yake juu ya taarifa potofu kuhusu virusi vya corona, lakini si mara ya kwanza kumuadhibu Bwana Trump kutokana na ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake.

Muda mfupi baadaye, kampuni ya Facebook ikafuta ujumbe ambao ulifanana na ule wa Twitter, kutoka kwa rais huyo wa Marekani.

Facebook ilifuta ujumbe huo wa sauti kutoka kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha habari cha Fox News – ikisema kuwa ujumbe huo una “ujumbe wenye madhara wa taarifa za kupotosha kuhusu Covid- 19 “.


EmoticonEmoticon