Google Wazindua Nearby Kwa Mfumo Wa Android Kama Apple

Kwa muda mrefu umekuwepo uvumi kuwa Google wapo mbioni kutoa kitu ambacho kinafanya kazi sawa na AirDrop ya Apple hatimae sasa sio uvumi tena bali ni kweli.

Hapo awali iliaminika kuwa huduma hii ingeitwa FastShare lakini jina limebadilika ingawa misingi ya kazi yake imebaki kuwa illeile na kwa sasa inapatikana  kwenye baadhi ya Google Pixel, simu za Samsung na hapo baadae kipengele hicho kitaweza kufanya kazi kwenye rununu zinazotumia Android 6 na kuendelea

Nearby Ni Nini?

Hiki ni kipengele kwenye simu za Android kuweza kutuma na kutokea vitu kutoka rununu moja kwenda nyingine. Simu janja mbili zinazotumia Android zinakuwa karibu na mtumiaji ana chagua kile ambacho kukituma kwenda kwenye simu ya pili. Mtu anayepokea anaweza kuudhisha/kusitisha mchakato wa kutokea kitu kutoka kwa anayekituma.

Kipengele hicho kikiwashwa kinampa uwezo wa kuchagua nani wa kumtumia aliyopo kwenye orodha ya majina ya watu aliwahifadhi, waliowaficha lakini hata kuweza kupokea kitu kutoka kwa mtu ambae hujamuhifadhi kwenye rununu.

Pia, kwenye Nearby Share mtu anaweza akaamua simu gani iwezekuiona au isiyonekane kabisa na inaelezwa kipengele hicho kitaanza kupatikana kwenye Chromebook ndani ya siku za usoni. Vilevile, kwenye maboresho ya hapo baadae kitu hicho kitaweza kufanya kazi kwenye Windows, iOS/macOS.


EmoticonEmoticon