Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi August 06

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi August 6, 2020

1. Mchakato wa winga wa Barcelona Philippe Coutinho kuhamia Arsenal unaelekea kukamilika. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil msimu uliopita alikuwa Bayern Munich kwa mkopo.

Pia Arsenal imetoa ofa ya miaka mitatu kwa winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31.

2. Chelsea iko katika mazungumzo ya hatua ya mwisho na beki wa kushoto wa Real Madrid Sergio Reguilon, 23, ambaye msimu uliopita alikuwa Sevilla kwa mkopo.

3. Mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen yuko tayari kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Uhispania. Hatua hiyo itakatisha tamaa Chelsea, ambayo ilikuwa inamfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 28,

4. Fulham itampa ofa kocha Scott Parker ya mkataba mpya baada kushinda kwenye mashindano ya michuano.

5. Mchezaji wa Real Madrid James Rodriguez, 29, amepangiwa kuhamia kwa mahasimu Atletico Madrid kwa kitita cha pauni milioni 13.5.


EmoticonEmoticon