Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa August 07

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa August 7, 2020

1. Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre -Emerick Aubemayang ,31, anakaribia kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo.

2. Barcelona inajiandaa kuwasilisha dau la £35.9m kwa beki wa Leicester mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uturuki Caglar Soyuncu.

3. Winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Arsenal utaogharimu £100,000 kwa wiki.

4. Lazio wana imani ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Manchester City David Silva . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu..

5. Manchester United itasikiza ofa za kumuuza kiungo wa kati wa England Jesse Lengard mwenye umri wa miaka 27 .


EmoticonEmoticon