Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne August 04

Philippe Coutinho
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne August 04

1. Arsenal pia iko makini kumfuatilia mchezaji wa Bayern Munich raia wa Brazil Philippe Coutinho, 28, na kiungo wa kati wa Atletico Madrid raia wa Ghana Thomas Partey, 27.

2. Winga wa Chelsea Willian, 31, amekataa mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo na amekuwa akifanya mazungumzo ya uhamisho wa bure kwenda Arsenal, ambayo iko tayari kutoa mkataba wa miaka mitatu kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kama anavyotaka mwenyewe.

3. Manchester United itahitajika kusubiri hadi kipindi cha mwisho kabisa cha usajili kumtafuta kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 24 wa Aston Villa.

4. Kocha wa Chelsea Frank Lampard ameshabaini walinzi watano tayari kuwauza na atafanya mikakati ya kumsajili Ben Chilwell, 23, beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza.

5. Manchester United inakaribia kumsajili winga wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho katika mkataba wa karibia miaka mitano. 


EmoticonEmoticon