Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne August 11

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne August 11, 2020

1. Manchester United wanaendelea na juhudi za kumsaka winga wa kimataifa wa England Jadon Sancho licha ya Borussia Dortmund kusisitiza kuwa nyota huyo wa miaka 20- atasalia katika klabu hiyo msimu ujao.

2. Aaron Ramsey hajamridhisha kocha Andrea Pirlo wa Juventus. Kingo huyo wa kati wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 29 yuko huru kuhamia klabu nyingine. 

3. Chelsea wamekubali kumpatia mkataba wa miaka mitano mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz lakini wamefahamishwa kuwa kiungo huyo wa miaka 21- atawagharimu £90m. 

4. Manchester City watapokea ada ya £8m kumuachilia mlinzi wa kati wa Argentina Nicolas Otamendi,32, msimu huu wa joto.

5. Inter Milan wanamlenga beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, wakati wa uhamisho.


EmoticonEmoticon