Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano August 05

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano August 5

1. Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, atapewa mkataba mpya wa pauni 100,000 wiki moja baada ya Manchester United kuonesha haina nia ya kutaka kumsajili.

2. Mabingwa wa Ligi ya Premier Liverpool inakaribia kumaliza mkataba wa pauni milioni 9 kwa mlinzi wa Aissa Mandi wa Real Betis na Algeria, 28.

3. Manchester City bado haijawasiliana na Barcelona kuhusu beki wa kulia Sergi Roberto, licha ya kuhusishwa kwa kiasi kikuwa na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania, 28, na haina mpango huo. 

4. The Reds pia inajitayarisha kwa dau la pauni milioni 10 kwa beki wa kushoto wa Norwich na Ireland Kaskazini Jamal Lewis, 22, wakati inatafuta nani wa kuvaa viatu vya Andy Robertson.

5. Leicester City wamefanya mazungumzo na Barcelona kuuliza ikiwa inaweza kumchukua mshambuliaji wa Ureno, 20, Francisco Trincao kwa misimu miwili ya mkopo, ikiwemo wajibu wa kumnunua kwa pauni milioni 45 (€50m) mwisho wa msimu.


EmoticonEmoticon