Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu August 10

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu August 10, 2020

1. Barcelona wanatumai kumshawishi kiungo wa kati Bernardo Silva, 25, aondoke Manchester City na wanaweza kumpatia ofa mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Ureno Nelson Semedo, 26, kama sehemu ya mkataba.

2. Mabingwa wa Primia Ligi Liverpool wanapanga kumuhamisha kiungo wa kati wa Wales David Brooks, 23, kwa pauni milioni 35 kufuatia kushushwa kwa daraja kwa timu ya Bournemouth.

3. Everton, Tottenham na West Ham pia wanania ya kusaini mkataba na Brooks.

4. Mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King analengwa sana na timu ya Ufaransa Paris St-Germain, huku hasimu wake wa Italia Lazio na Roma wakiwa wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 28.

5. Uwezekano wa Tsimikas wa kuhamia Liverpool ni pigo kwa Leicester, ambao walikua wamempanga kama mchezaji atakayechukua nafasi ya Ben Chilwell, 23, iwapo kiungo huyo wa safu ya nyuma -kulia angeondoka kujiunga na Chelsea msimu huu.


EmoticonEmoticon