Habari Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi August 13

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi August 13, 2020

1. Manchester City wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati wa Bayern Munich Muhispania Thiago Alcantara na wanaaminiwa kutoa ofa ya malipo zaidi ya Liverpool kwa ajili ya kumpata kijana huyo mwenye umri wa miaka 29.

2. Watford wako tayari kudai rekodi ya garama ya zadi ya pauni milioni 40 kwa winga Msenegal Ismaila Sarr, 22, huku Liverpool na klabu nyingine za Ulaya zikitangaza nia yao ya kumchukua.

3. Roma wanaweza kumbadilisha kiungo wa kati Mguinea Amadou Diawara mwenye umri wa miaka 23 na kiungo wa kati Arsenal Lucas Torreira ambaye ni raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka , 24. 

4. Juventus wamewasiliana na Arsenal juu ya uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, mwenye umri wa miaka 29.

5. Manchester United wamesitisha kwa muda biashara ya kuwahamisha wachezaji huku wakijaribu kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20. 


EmoticonEmoticon