Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu August 3

Mikel Arteta
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu August 3

1. Washindi wa kombe la FA Arsenal wanamlenga beki wa kati wa Brazil Diego Carlos huku Mikel Arteta akipanga marekebisho makubwa msimu ujao.

2. Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda. 

3. Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania.

4. Arsenal itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo.

5. Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil, 22. 


EmoticonEmoticon