India Yapiga Marufuku Programu Ya TikTok

 

Serikali ya India imepiga marufuku programu maarufu ya TikTok pamoja na programu nyingine nyingi zilizotengenezwa na Wachina ikisema ni hatari kwa nchi hiyo

Mbali na TikTok, jumla ya programu 59 zimepigwa marufuku, ikiwemo programu maarufu ya ujumbe ya WeChat, Weibo, Mitandao ya biashara (e-commerce) kama Alibaba, Shein na nyingine nyingi.

Taarifa kutoka Wizara ya Habari na Teknolojia inasema imezifunga jumla ya programu tumishi 59 ikiwemo WeChat, Weibo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa vyanzo anuwai kwamba zinaiba na kusambaza data za watumiaji kwa njia isiyoidhinishwa.

India ni soko kubwa la nje ya Uchina la TikTok; ina wastani wa watumiaji milioni 120.


EmoticonEmoticon