J Cole Afanya Mazoezi Kwaajili Ya Kuingia Kwenye Ligi Ya NBA

J Cole
Kwa mujibu wa Master P, J Cole ameanza mazoezi kwa ajili ya kupata nafasi kwenye ligi hiyo maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani. 

Juzi Jumamosi (Aug. 1) mtandao wa TMZ ulirusha mahojiano na mwanzilishi huyo wa No Limit Records ambapo aliweka wazi juu ya hilo

"Nilipozungumza na J. Cole, alisema 'Unajua, mzee wewe ulishawahi kufanya. Unafikiria vipi kama na mimi nifanye?" alisimulia Master P ambaye pia aliwahi kucheza kwa uchache kwenye NBA akiwa na Toronto Raptors na Charlotte Hornets miaka ya 90.

"Kupata moja ya hizi jezi za NBA haiwezi kuwa kitu rahisi, kutakuwa na chuki sana, kutakuwa na watu wengi sana ambao watashindwa kukuamini. J. Cole amepata size inayomtosha, yupo gym kwa sasa." alimaliza Master P.


EmoticonEmoticon