Juventus Yamfuta Kazi Aliyekuwa Kocha Wao Maurizio Sarri

Miamba ya Soka ya Jiji la Turin Klabu ya Juventus imemfuta kazi meneja wake Maurizio Sarri baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu Mmoja.

Sarri amewaongoza Juventus Kutwaa taji la tisa mfululizo la ubingwa wa Ligi ya Italia Seria A, lakini vibibi vizee hao wakaondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya kumi na Sita bora na Wafaransa Wa Lyon.

Juventus Walishinda kwa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa siku ya Ijumaa lakini Lyon walisonga mbele kwa faida ya Goli la ugenini.

Sarri Mwenye miaka 61 alipewa jukumu la kuinoa Juventus kwa Miaka mitatu msimu uliopita akitokea klabu ya Chelsea ya nchini England. Sarri alichukua nafasi ya Massimilliano Allegri mwezi June 2019

Kocha wa Kikosi cha vijana na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Andrea Pirlo, anatajwa kuwa mmoja ya watu wanaopewa nafasi ya kuwa Kocha mpya wa Timu hiyo makocha wengine wanaopigiwa chapuo la kuwanoa vibibi hao wa Turin ni Zidane wa Real Madrid na Meneja wa Zaman wa Spurs Mauricio Pochettino.


EmoticonEmoticon