Kampuni Iliyoipa Pombe Jina La Nywele Za Sehemu Za Siri Waomba Radhi

Watengenezaji wa pombe nchini Canada wamelazimika kuomba msamaha kwa kuipatia pombe jina ambalo katika jamii ya Maori kwa kawaida hutumiwa kutaja ''nywele za sehemu za siri''.

Watengenezaji wa pombe wa kampuni ya Hell's Basement Brewery mjini Alberta walisema kuwa walitangaza kinywaji chao kwa jina la Huruhuru miaka miwili iliyopita, wakidhani neno hilo lina maanisha "manyoya".

Lakini mtangazaji maarufu wa kituo cha televisheni cha kabla la Maori-Hamua Nikora alieleza maana ya neno hilo kupitia video aliyotuma kwenye Facebook, kudhihirisha kuwa kweli neno Huruhuru linamaanisha ''nywele za sehemu za siri''katika jamii ya Maori.

Muasisi wa kampuni hiyo ya kutengeneza bidhaa za pombe aliwaahidi watu wa Maori kuwa bidhaa hiyo sasa itapatiwa nembo mpya ya kuinadi.

"Tunakubali kwamba hatukuzingatia matumizi ya kawaida ya neno huruhuru linalomaanisha nywele za sehemu za siri, na tungefanya mashauriano na wawakilishi wa Maori tungeweza kuelewa vema kuliko kutumia kutegemea kamusi za mitandaoni ," Mike Patriquin aliuambia mtandao wa habari wa CBC.

Tungependa kueleza bayana kwamba haikua nia yetu kukiuka maadili, au kuukera utamaduni wa Maori ama watu wake kwa njia yoyote ile, kwa wale wanaoihisi kuwa wamevunjiwa heshima, tunaomba msamaha ."


EmoticonEmoticon