Kampuni Ya Microsoft Kuinunua TikTok Ya China, Ni Baada Ya Marufuku Ya Trump

Microsoft Tik Tok
Mwasisi wa kampuni ya teknolojia ya Bytedance ambayo ndio mmilki wa mtandao wa kijamii wa Tik Tok, amesema wanafanya jitihada kuhakikisha wanapata matokeo mazuri, wakati huu ambapo mazungumzo yanaendelea kuhusiana na kuuzwa kwa operesheni zake za Marekani kwa kampuni ya Microsoft.

Tik Tok ambayo ni maarufu sana miongoni mwa vijana Marekani na kote Duniani ndio mtandao wa hivi karibuni unaolengwa katika mzozo wa kibiashara kati ya China na Marekani.

Marekani imesema kampuni hiyo inayomilikiwa na Mchina, ni kitisho cha usalama wa Taifa wa Marekani (kwa kudukua taarifa za watumaji), jambo ambalo Tik Tok inakanusha, Rais Trump amewapa siku chache Tiktok kumaliza mazungumzo na microsoft ili Kampuni hiyo isimamiwe na Wamarekani badala ya Wachina na kusema wakishindwa ataufuta mtandao huo Marekani.

Microsoft imesema kwamba itaendelea na mazungumzo ya kununua operesheni Tik Tok Marekani, Tik Tok inakadiriwa kuwa na watumiaji Bilioni moja kote Duniani.


EmoticonEmoticon