Kampuni Ya Twitter Kununua Mtandao Wa TikTok

Kampuni ya Twitter imeripotiwa kuwa ipo kwenye mazungumzo ya kuununua mtandao wa TikTok.


Mtandao wa Wall Street Journal umeripoti, Twitter na TikTok wapo kwenye mazungumzo ya awali kuhusiana na biashara hiyo. 

Licha ya taarifa hiyo, mtandao wa WSJ pia bado unaripoti kwamba kampuni ya Microsoft ina kipaumbele kikubwa katika mbio za kuinunua TikTok.


Kuuzwa kwa mtandao wa TikTok kumekuja baada ya tamko la Rais Donald Trump kwamba ataupiga marufuku mtandao huo nchini Marekani, vinginevyo ununuliwe na kampuni yoyote ya Kimarekani. Vitisho vya Trump viliambatana na maelezo ya kwamba TikTok ni tishio kwa usalama.


EmoticonEmoticon