Kesi Ya R Kelly Wengine Watatu Wamekamatwa Na Kushtakiwa

Watu watatu wamekamatwa na kushitakiwa kutokana na kuhusika kujaribu kuwapa Rushwa pamoja na kuwatishia Maisha wanawake ambao walimshitaki R.KELLY kwenye kesi yake inayomkabili ya Unyanyasaji wa Kijinsia .

Kwa Mujibu wa NBC News New York , watu hao wanaohisiwa kuwa na ukaribu na Nguli huyo wa R&B walijaribu kutega kitu Chenye asili ya Bomu katika gari la Baba wa mmoja wa wanawake ambao wamemshitaki R. Kelly .

Shitaka hilo lililofunguliwa na Mwanasheria wa Wanawake hao , Limewataja watu hao kuwa ni Richard Airlines , Donnell Russell na Michael Williams ambao wote wana uhusiano wa Karibu na Mwanamuziki R. Kelly .

“Kwa Vitu vilivyojaribu kuvifanya watu hawa , inaonyesha wazi kuwa wanaweza kufanya tukio lolote bila hofu ili kumsaidia R.kelly katika kesi hii” - aliongea Wakili wa Wanawake waliomshitaki R.kelly Mr. Peter Fitzhugh

Licha ya ushahidi Mkubwa kuthibitisha kuwa R.kelly alihusika katika makosa mbalimbali ya unyanyasaji wa Kijinsia , Lakini mpaka hivi sasa Nguli huyo wa Muziki ameendelea kukana Mashitaka yote yanayomkabili .


EmoticonEmoticon