Maandamano Yaendelea Kupamba Moto Lebanon

Raia wa Lebanon wameendelea kuandamana kuipinga Serikali yao kwa madai ya uzembe uliosababisha mlipuko Bandari ya Beirut ulioua zaidi ya watu 150. 

Hatua hii inakuja kufuatia Serikali kusema mlipuko huo umetokana na Tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate zilizohifadhiwa Bandarini hapo huku taarifa nyingine zikidai huenda eneo hilo limepigwa Bomu. 

Zaidi ya Watu 700 wamejeruhiwa hadi sasa kufuatia maandamano hayo huku wengine wakihofiwa kufariki Dunia.


EmoticonEmoticon