Maelfu Ya Watu Wamuunga Mkono Didier Drogba Baada Ya Kuwasilisha Fomu Za Kuwania Nafasi Ya Uraisi

Didier Drogba
Maelfu ya watu wajikusanya nje ya afisi za Soka katika taifa Ivory Coast pale mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Didier Drogba alipokuwa anawasilisha karatasi zake za kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka la taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Drogba wa miaka 42 ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ni miongoni mwa wawaniaji wanne ambao wanataka kuwa vinara wa shirikisho la soka la  taifa hilo.
Didier Drogba
Kando na kupata uungwaji mkono wa vilabu vitatu kati ya vilabu 14 vinavyoshiriki  ligi kuu ya taifa hilo, ni sharti mchezaji huyo wa zamani apate uungwaji mkono wa vilabu viwili vinavyoshiriki katika ligi ya daraja ya pili na pia kuungwa mkono na watu  watano kutoka vitengo tofauti vikiwemo Makocha, Madaktari, uongozi wa sasa wa shirikisho hilo na wachezaji wenza wa zamani wa taifa hilo pamoja na waamuzi.

Drogba aliwasilisha karatasi zake mida ya saa  kumi na moja jioni na kupokelewa na mashabiki wake waliokuwa wanamngoja nje ya afisi kuu za shirikisho la michezo katika taifa hilo.


EmoticonEmoticon