Marekani Yatoa Tahadhari Ya Usafiri Kenya Kufuatia Ongezeko La Maambukizi Ya Corona

Marekani imetoa tahadhari dhidi ya usafiri wa Kenya baada ya idadi ya maambukizi ya corona kuongezeka nchini humo.

Taarifa katika tovuti ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya umesema serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya kukaa nyumbani na kurejesha usafiri na baadhi ya shughuli za kibiashara.

Kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti magonjwa-CDC, inaonekana kuwa kuna kiwango kikubwa cha maambukizi kwa wasafiri na hakuna angalizo la kupunguza tatizo hizo. Wakati huohuo Kenya imetangaza kuwa sekta ya utalii imepoteza mabilioni ya dola katika pato la taifa kuanzia Januari mpaka sasa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Credit:Bbc


EmoticonEmoticon