Mchungaji TB Joshua Anasubiri Sauti Toka Kwa MUNGU Kabla Ya Kurejesha Huduma Yake

Mchungaji maarufu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua anasema anasubiri kusikia 'sauti ya Mungu' kabla hajafungua huduma za ibada katika jiji la biashara la Lagos.

Mamlaka mjini Lagos imeruhusu huduma ibada kuanza siku ya Jumapili kuanza,waumini wakiwa nusu yake baada ya kufungwa kwa huduma hizo kwa miezi kadhaa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Katika video aliyoiweka kwenye kurasa yake ya Twitter, TB Joshua alisema amesikia kutoka kwa mamlaka lakini bado anasubiri kusikia kutoka kwa Mungu.

"Muwe na uhakika kuwa punde tu nitakaposikia sauti ya Mungu , nitawajulisha huduma za ibada zitaanza lini," aliongeza.

Mapema mwaka huu nabii huyo alisababisha mkanganyiko baada ya kudai kuwa mlipuko wa virusi vya corona utaisha tarehe 27,Machi.siku chache kabla ya marufuku ya kutoka nje haijaanzishwa katika jimbo la Lagos, Ogun na mji mkuu Abuja.

"Mwishoni mwa mwezi huu, tupende au tusipende, haijalishi kama dawa gani itatengenezwa kwa ajili ya kutibu, virusi hivi vitaondoka kama jinsi vilivyokuja," alisema hayo katika mahubiri yake.

Tarehe 27 Machi ilipopita alijikuta anadhihakiwa kwa maono ya uongo.

Lakini alijitetea kwa kusema kuwa alimaanisha virusi vitaanza kuisha kule vilipoanzia mjini Wuhan nchini China,na tayari vimeondoka."


EmoticonEmoticon