Mlipuko Beirut Wawaua Watu 78 Na Kusababisha Uharibifu Mkubwa

Lebanon inaomboleza baada ya mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Beirut kuwaua watu 78 na kuwajeruhi wengine 4000 siku ya Jumanne.

Mji wote uliyumbishwa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari kabla mlipuko huo uliofanana na wingu la uyoga kutokea.

Rasi Michel Aoun alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.

Aliitisha kikao cha dharura siku ya Jumatano , na kusema hali ya dharura ya wiki mbili imetangazwa.

Rais Aoun pia alitangaza kwamba serikali itatoa $66m za hazina ya dharura. ''Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa'' , alisema mkuu wa kundi la msalaba mwekundu George Kettani akizungumza na vyombo vya habari. ''Kuna waathiriwa kila mahali''.


EmoticonEmoticon