Mwanamfalme Wa Saudi Ashtumiwa Kwa Njama Ya Mauaji Canada

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa wa ujasusi wa Saudi.

Mpango huo wa kumuua Saad al-Jabri ambao haukufanikiwa ulifuata muda mfupi baada ya mauaji ya mwanahabari aliyeuawa nchini Uturuki, Jamal Khashoggi, nyaraka zilizowasilishwa katika mahakama ya Marekani zimedai.

Bwana Jabri, afisa mstaafu wa serikali ya Saudi Arabia, alikimbilia ughaibuni miaka mitatu iliyopita.Tangu wakati huo amekuwa akipewa ulinzi binafsi mjini Toronto.

Mpango huo wa mauaji inasemekana kuwa ulifeli baada ya maafisa wa mpaka wa Canada kuanza kushuku kikosi hicho walipokuwa wanajaribu kuingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Toronto Pearson, nyaraka zilizowasilishwa mahakamani zinaonesha.

Kwa miaka mingi, Bwana Jabri, 61, alikuwa kiungo muhimu katika huduma ya ujasusi ya siri Uingereza na mashirika mengine ya kijasusi ya nchi za Magharibi nchini Saudi Arabia.


EmoticonEmoticon