Nas Aongelea Mahusiano Kati Yake Na Rapa Jay Z

Baada ya wengi kuanza kusema kwamba huwenda bifu kati yao bado linaendelea, Nas ameizungumzia ishu ya Jay-Z kuachia ngoma kila baada ya ujio wake.

Wiki hii Nas ameachia album yake mpya "King's Disease" lakini siku kadhaa nyuma kabla ya kuiachia, Jay-Z na Pharrell Williams waliachia mkwaju mpya "Entrepreneur" ambapo wengi walikuja na kauli kwamba Jay amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara Nas akitaka kuachia kazi.

Sasa kwenye mahojiano na The Breakfast Club, Nas amejibu kwa kusema hafikirii kama ni bifu kati yao bali ni bahati mbaya tu wamekuwa wakigongana kwenye uachiaji kazi.

Kwenye mahojiano hayo pia, Nas alijibu kwanini hakuwahi kufanya ngoma yoyote na The Notorious B.I.G , alisema kuna siku walikuwa studio pamoja wakitaka kufanya ngoma kadhaa ikiwemo remix ya "Gimme The Loot" lakini waliishia kuvuta bangi kwa wingi kiasi cha kuwafanya kuwa "High" na walipokuja kuzinduka walijikuta wamechoka sana kiasi cha kushindwa kufanya chochote.


EmoticonEmoticon