Orodha Ya 10 Bora Waigizaji Wanaoingiza Pesa Nyingi 2020 Forbes

The Rock ameongoza kwenye orodha ya Waigizaji wa kiume ambao wamelipwa/wameingiza pesa nyingi kwa mwaka 2020 kwa muijbu wa Jarida la Forbes.

Orodha hiyo (Highest Paid actors of 2020) ya kuanzia June 2019 hadi June 2020, imemtaja kwa mara ya pili mfululizo The Rock kama kinara huku akiwa ametengeneza kiasi cha Dola za Kimarekani ($87.5M) ambazo ni sawa na zaidi ya TSH. Bilioni 200.

Baadhi ya pesa alizotengeneza ni lile dili la ($23.5M) kwa kuuza filamu ya Red Notice kwenye kampuni ya Netflix. Kiasi kingine kimeingia kupitia bidhaa yake ya mavazi ya kufanyia mazoezi na bidhaa zingine.

TOP 10
1. The Rock - $87.5M
2. Ryan Reynolds - $71.5M
3. Mark Wahlberg - $58M
4. Ben Affleck - $55M
5. Vin Diesel - $54M
6. Akshay Kumar - $48.5M
7. Lin-Manuel Miranda - $45.5M
8. Will Smith - $44.5M
9. Adam Sandler - $41M
10. Jackie Chan - $40M


EmoticonEmoticon