Raisi Wa Marekani Atoa Siku 45 Kabla Hajazuia Mitandao Ya Kijamii TikTok Na WeChat

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa ndani ya siku 45 zijazo atazuia mitandao ya kijamii ya TikTok na WeChat inayomilikiwa na Wachina kama isipouzwa kwa Wamarekani ndani ya siku hizo.

Trump amepanga kuzuia mitandao hiyo Septemba 15, ikiwa haitauzwa. Aidha, Wahusika wa mitandao hiyo wapo katika maongezi na kampuni ya kimarekani ya Microsoft.

TikTok ina watumiaji zaidi ya milioni 100 nchini Marekani. Azma ya Rais Trump kuifunga mitandao hiyo imetokana na tuhuma za kuiba taarifa za watumiaji wake na kupeleka kwa Serikali za China.


EmoticonEmoticon