Raisi Wa Marekani Kujiunga Na Viongozi Wengine Kuzungumzia Lebanon

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atajiunga na mkutano kwa njia  ya simu pamoja na rais wa Lebanon na viongozi wengine wa  dunia siku ya Jumapili kujadili msaada kwa Lebanon kutokana na mripuko uliotokea mjini Beirut.

Trump alisema kupitia Twitter kuwa  alizungumza  binafsi katika  nyakati tofauti  na  rais wa Lebanon  Michel Aoun na rais wa Ufaransa  Emmanuel  Macron, ambae pia  atajiunga na  mazungumzo hayo ya simu. 

Alisema  amemwambia Aoun kuwa  ndege  kubwa   tatu za Marekani  zimo  njiani kwenda  Lebanon  kupeleka  madawa, chakula, maji na madaktari.

Trump  na  Macron walizungumza  kwa simu  na  walieleza masikitiko  yao  makubwa  kutokana na  upotevu wa maisha  na uharibifu  mjini  Beirut, msemaji  wa  Ikulu  ya Marekani Judd Deere alisema katika  taarifa.

Rais wa Lebanon  hata  hivyo  amekataa uchunguzi wa kimataifa  kuhusiana  na  maafa ya mripuko mjini Beirut, akisema  kombora  ama  uzembe unaweza  kuwa  chanzo cha mripuko huo wakati waokoaji wanatafuta bila kuchoka watu walionusurika.


EmoticonEmoticon