Raisi Wa Ufilipino Arudia Tena Kauli Yake, Watu Watumie Petroli Kuosha Barakoa

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema kwa mara nyingine tena kuwa watu watumie petroli kuosha barakoa - na kusisitiza kwamba hafanyi mzaha.

Alisema maneno kama hayo wiki iliyopita lakini maafisa walimrekebisha haraka sana na akasema kwamba huo ulikuwa mzaha.
Maafisa wa afya wanasema kuwa barakoa zilizotengenezwa kwa kitambaa cha nguo zinatakiwa kuoshwa kama kawaida na zile barakoa zingine zitumike mara moja tu na kutupwa.
Lakini Ijumaa, rais huyo alisisitizia matamshi yake na kuongeza "kile nilichosema ni ukweli… nendeni kwenye kituo cha petroli".
Hakuna ushahidi wowote kwamba petroli inaweza kutumiwa kuua vijidudu kwenye barakoa; na kuitumia kwa muda mrefu kunaweza kusababisha hatari na kuinyunyizia vioevu kunaweza kusababisha moto.
Duterte alisema nini?
Akirejelea matamshi yake ya awali, Bwana Duterte alisema: "Wakosoaji wanasema, 'Duterte ana kichaa.' Ni mpumbavu! Ikiwa mimi ni mpumbavu, wewe unastahili kuwa rahisi, sio mimi.
"Kile nilichosema ni cha kweli. Ikiwa pombe haipatikani, hasa kwa maskini, nenda tu kwenye kituo cha petroli, na utumie petroli kuua vijidudu.
"Sio utani. Sio mzaha. Wewe… wewe jitahidi kuwa na mawazo kama yangu."


EmoticonEmoticon