Serikali Ya Lebanon Yajiuzulu

Serikali ya Lebanon imejiuzulu huku ghadhabu ya umma ikiendelea kupanda nchini humo juu ya mlipuko uliotokea Jumanne ulioharibu sehemu ya mji wa Beirut na kuwaua watu 200.

Tangazo la kujiuzuli lilitolewa katika televisheni ya taifa na Waziri Mkuu Hassan Diab Jumatatu usiku.

Watu wengi wameiutuhumu uongozi wa nchi kuhusika na mlipuko huo kwa madai ya uzembe na ufisadi.Waandamanaji wameingia mitaani na kukabiliana na polisi kwa siku ta tatu mfululizo.

Mlipuko mkubwa ulisababishwa na kulipuka kwa tani 2,750 za mbolea ya ammonium nitrate iliyowekwa bila kuzingatia usalama kwenye ghala kwa miaka kadhaa bila

Rais Michel Aoun ameiomba serikali iendelee kushikilia mamlaka kwa muda hadi pale serikali mpya itakapoundwa.


EmoticonEmoticon