Shirika La Afya Duniani Lasema Janga La Maambukizi Ya corona Kuwa La Muda Mrefu

Shirika la afya duniani WHO limeonya kwamba janga la maambukizi ya corona linaelekea kuwa la muda mrefu baada ya kufanya kikao cha kutathmini kiwango cha maambukizi.

Kamati ya shirika hilo la afya imekutana kwa mara ya nne ,tangu kulipuka kwa maambukizi miezi sita iliyopita na kupiga mbiu ya mgambo duniani kote. 

Kamati hiyo pia imetahadharisha juu ya hatari inayoweza kutokea endapo nchi zitaacha kuchukua hatua za kupambana na maambukizi na pia kwa sababuya kubanwa kijamii na kiuchumi.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la corona litakuwapo kwa muda mrefu. Amekumbusha kuwa maradhi hayo yalipotangazwa kuwa janga la kimataifa, watu walioambukizwa hawakuzidi mia moja na hakuna waliokufa wakati huo nje ya China. 

Shirika la afya duniani limelaumiwa na Marekani kwa kuchelewa kuutangaza ugonjwa huo wa homa ya mapafu kuwa janga la kimataifa iliyodai kwamba shirika hilo linaegemea sana upande wa China. 

Marekani ilitangaza ilijiondoa rasmi kutoka kwenye shirika hilo mnamo mwezi wa Julai


EmoticonEmoticon