Tafiti Zinasema Takribani 800 Wamekufa Kutokana Na Taarifa Potufu Za Corona

Takriban watu 800 wamekufa kote duniani kutokana kwasababu ya taarifa potofu zinazohusiana na virusi vya corona katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, wanasema watafiti.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Marekani linaloandika taarifa za magonjwa ya maeneo yajito na usafi, unasema kuwa watu wapatao 5,800 walilazwa hospitalini kutokana na taarifa zisizo sahihi juu ya corona zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wengi walikufa kutokana na kunywa kemikali ya methanol au bidhaa nyingine za kuua viini hatari.

Waliamini kimakosa kwamba bidhaa hizo ni tiba ya virusi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) awali lilisema kuwa "janga la taarifa" zinazozingira Covid-19 husambaa haraka sawa na virusi vyenyewe, huku nadharia potofu, uvumi na unyanyapaa wa kitamaduni vyote kwa pamoja vikichangia vifo na majeraha


EmoticonEmoticon