Trump Anuia Kumuondoa Waziri Wa Ulinzi Kufuatia Tofauti

Rais Donald Trump wa Marekani amefanya majadiliano binafsi na washauri wake kuhusu uwezekano wa kumuondoa waziri wa ulinzi Mark Esper, baada ya uchaguzi mkuu wa Novemba baada ya kuongezeka kwa tofauti baina yao.

 Taarifa hii ni kulingana na chanzo chenye uelewa na mjadala huo wa ndani hapo jana.Chanzo hicho kimesema kwa sharti la kutotajwa jina kwamba wawili hao hawaelewani, lakini Trump hakutaka kumuondoa Esper hadi baada ya uchaguzi wa Novemba 3.

 Esper anaheshimiwa na Republican na Democrat kama muhimili imara ndani ya Pentagon, lakini Trump hakuridhishwa na alivyopingana naye kwenye suala la kukiuka sheria ya uasi dhidi ya serikali kwa kupeleka wanajeshi kukabiliana na machafuko ya raia yaliyoibuka mwezi Juni baada ya kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi wa Minneapolis, huku mwezi uliopita akitofautiana na Trump kwa kuzuia bendera za majimbo kupepea kwenye maeneo ya kijeshi.


EmoticonEmoticon