Trump Atoa Kauli Baada Ya Mlipuko Uliotokea Huko Lebanon, Ni Shambulizi Lililopangwa

Rais Donald Trump amesema anaamini mlipuko uliotokea Beirut Lebanon ni shambulizi lililopangwa na kwamba Bandari hiyo imelipuliwa kwa Bomu au silaha nyingine nzito “sina maelezo zaidi lakini nimeongea na Majenerali wa Jeshi wa Marekani na mtazamo wao unaamini hilo ni shambulizi”

Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab amesema taarifa za awali zimeonesha chanzo cha mlipuko uliosababisha vifo vya zaidi ya Watu 70 Bandari ya Beirut ni kulipuka kwa Ammonium Nitrate Tani 2750 iliyohifadhiwa Bandarini, inaaminika kemikali hiyo imelipuka kutokana na cheche za moto wakati wa kuchomelea mlango (welding), bado wengi wameonekana kutokubaliana na sababu hiyo wakiamini Majengo yamelipuliwa kwa Bomu au silaha nyingine.


EmoticonEmoticon