Uchaguzi Wa Marekani : China,Urusi, Iran Zinajaribu Kuweka Ushawishi Kwenye Kura

China, Urusi na Iran ni kati ya nchi zinazotaka kushawishi uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu, mkuu wa idara ya intelijensia nchini Marekani ametahadharisha.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara hiyo ilisema nchi za kigeni zilikuwa zinatumia ''njia za ushawish'' kuyumbisha kura.

Ilisema China haikutaka kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump huku Urusi nayo ilitaka kumuumiza Joe Biden wa Democrat. Wakuu wa ujasusi wanaishutumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Wanasema Urusi ilitaka kusaidia kuongezea nguvu kampeni ya Bw Trump,ikiwemo kueneza habari za uongo mtandaoni. Urusi imekana madai hayo.

Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa alichopanga kufanya kuhusu ripoti kuhusu kuingilia uchaguzi, Rais Trump alisema utawala wake utaangalia "kwa karibu" suala hilo.


EmoticonEmoticon