Ugonjwa Usio Wa Kawaida Wabainika Marekani

Watu wameombwa kuwa katika tahadhari kwa ugonjwa usio wa kawaida unaosambaa kwa kuumwa na kupe baada ya kubainika kwa mara ya kwanza Uingereza.

Wizara ya Afya imesema kwamba hatari iliyopo kwa umma ni ya chini lakini ni muhimu wawe waangalifu kuhusu kupe hasa wanapokuwa kwenye maeneo ya bustani msimu wa joto.
Ugonjwa huo unasababishwa na vimelea ambavyo vinaathiri chembe nyekundu za damu.
Mgonjwa wa pili aliyeambukizwa ugonjwa huo ambao ni nadra sana kutokea amegunduliwa.
Ugongwa huo unaosambazwa na kupe unaosababisha ubongo kufura mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi.
Dkt. Katherine Russell kutoka wizara ya afya amesema ugonjwa huo ni nadra sana na hivyo basi uwezekano wa maambukizi ni wa chini mno.
"Kupe hupatikana sana kati ya msimu wa kuchipua na pukutizi, kwahiyo ni muhimu ikiwa raia watachukua tahadhari ya juu ili kuhakikishi hawaumwi na kupe wanapokuwa nje wakijivinjari. 
Na pia tafuta ushauri wa daktari unapoanza kusikia vibaya baada ya kuumwa na kupe."


EmoticonEmoticon