Wagombea Wa Uraisi Marekani Joe Biden Na Kamala Harris Wamshambulia Trump

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden na mgombea mwenzake Kamala Harris wamemshambulia rais Donald Trump wakisema anapenda "kulalamika" na kuongeza kuwa ni kiongozi asiyefaa aliyeiacha Marekani katika "hali mbaya".

Wawili hao walifanya kampeini ya kwanza pamoja siku moja baada ya Bwana Biden kumzindua Bi. Harris kama mgombea mwenza.

Rais Trump amejibu tamko lao kwa kusema Bi Ms Harris "ameanguka kama jiwe" katika jaribio lake la kuwania urais.

Biden atamenyana na Trump, wa Republican, katika kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mwezi Novemba.

Credit:Bbc


EmoticonEmoticon