Walioambukizwa Virusi Vya Korona Duniani Wapindukia Milioni 18

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona ulimwenguni imepindukia milioni 18, kwa mujibu wa takwimu rasmi kufikia saa sita usiku wa kuamkia leo. 

Milioni moja kati yao wamesajiliwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Zaidi ya nusu ya watu walioambukizwa wapo nchini Marekani, Amerika ya Kusini na eneo la Karibiani. 

Marekani ndilo taifa lililoathirika vibaya zaidi likiwa na takribani watu milioni 4 laki 6 na 58 elfu. 

Tayari taifa hilo kubwa kiuchumi na kijeshi duniani limeshapoteza watu 154,793 kwa maradhi ya COVID-19, likifuatiwa na Brazil yenye watu milioni 2, laki 7 na 34 walioambukizwa na vifo 94,104. 

Nchi ya tatu duniani kukumbwa zaidi na virusi vya korona ni India yenye wagonjwa milioni 1,750,723 na vifo 37,364. Idadi ya waliosajiliwa kupoteza maisha kwa maradhi hayo duniani, imefikia sasa 687,941.
Credit:DW


EmoticonEmoticon